Msaada wa kisheria

Kliniki za huduma za kisheria ya RCK ambazo hufanyika katika afisi zao zinazopatika LWF, Kakuma 4 na Kalobeyei kwa sasa zimesimamishwa kwa sababu ya COVID-19. Wakimbizi na wanaotafuta hifadhi bado wanaweza kupata ushauri wa kisheria na usaidizi kupitia njia ya bure (0800 720 262) na simu ya ofisini (0701 414 978). Wasaidizi wa kufuatilia huduma ya ulinzi ambao ni wafanyikazi wa RCK huko Kakuma na Kalobeyei wanasaidia katika utambuzi wa kesi na rufaa.

Ufuatiliaji wa kizuizini unaendelea katika vituo vya polisi vya Kakuma na Kalobeyei kupitia ziara za wasaidizi wa kufuatilia huduma ya ulinzi. RCK inaendelea pia kufuatilia michakato ya korti.Ufuatiliaji wa kizuizini na michakato ya korti, ambayo inazingatia hatua za kuzuia COVID-19, inaendelea.

Kwa habari juu ya aina tofauti za nyaraka (vyeti vya kuzaliwa, ndoa na talaka, vyeti vya kifo, n.k.) tafadhali nenda kwa Hati (documentation).

Kwa nyaraka zinazohusu biashara yako, pamoja na vibali vya kufanya kazi, usajili wa biashara na vibali vya biashara, tafadhali nenda kwa ukurusa wa riziki (livelihoods).


See also

<< Back to Kenya homepage >> Select another country on our Help page