Elimu

Umoja Wa Kimataifa wa Wakimbizi (UNHCR) kupitia washirika yake wa Elimu, Shirikisho la Ulimwengu la Kilutheri (LWF), Finn Church Aid (FCA) na Windle International Kenya (WIK), hutoa elimu katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma na Makaazi ya Kalobeyei. 

Shule zitafunguliwa kwa usalama kwa muhula wa kwanza wa mwaka 2021, tarehe 26 Julai kulingana na miongozo ya Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya. UNHCR na washirika wake wameweka hatua muhimu za usalam za COVID-19,  kama vile barokoa, utumiaji wa vifaa vya thermo, kudumisha umbali wa kimwili vituo vya kunawa mikono na maji bomba. 

TAREHE ZA MUHULA WA SHULE 2021 

  • Muhula wa kwanza – 26 Julai  – Oktoba 2021 
  • Muhula wa pili – 1-10 Oktoba – 23 December 
  • Muhula wa tatu – 3 Januari – 26 Machi 

Elimu Za Shule Ya Msingi: Shule ya msingi  kambini ni bure na ya lazima. Mtoto yeyote anaweza kujiunga na shule ya msingi iliyo karibu wakato wowote wa kipindi cha shule, na vifaa vya kujifunzia na sare za shule zitatolewa, ingawa ni chache.  

Shule Za Mabweni: Kuna shule mbili za mabweni za wasichana,shule ya msingi ya Angelina Jolie na shule ya upili ya Morneau Shapell. Nafasi zinapewa wanafunzi amboa walipata alama zinazohitajika.Unaweza kuomba kulingana na alama zako, ulinzi na vigezo vya umri. Unaweza kupata maelezo zaidi wakati wito wa maombi utakapotolewa kila mwaka wa masomo.  

Shule Za Upili: Kwa sababu ya rasilimali chache, kila mwanafunzi anatakiwa kutoa Shillingi 3000 kila mwaka.  Ikiwa una maswali yoyote tafadhali wasilianna na Bodi ya usimamizi ya shule ya upili iliyoko karibu nawe.  

Udhamini wa Vyuo Vikuu: Udhamini wa elimu ya Juu uliopo ni mdogo na unapewa wanafunzi ambao wamefaulu mitihani na kufanya vyema. Kawaida hutangazwa katika bodi za matangazo kote kambini na washirika tofauti.   

Kitovu cha Elimu Magharibi mwa Turkana: Kitovu cha elimu cha magharibi cha Turkana kitaanza kutumika hivi karibuni. Kitovu kitawezesha vijana kupata fursa za elimu ya juu kupitia njia mchanganyiko. Habari zaidi itapatikana kupitia njia anuwai za mawasiliani 

Vitambulisho Vya Njiani Vya Wanafunzi: Wanafunzi wanoarudi shuleni wanapaswa kutembelea ofisi ya meneja wa Kambi ya RAS ili waweze kupewa vitambulisho vya njiani vitakavyo wawezesha kusafiri salama. Unaweza kuomba kuonana na Mkuu wa Kambi kwenye ofisi yake kupitia KASI katika eneo za wazi (field post) za UNHCR