Kulinda Haki za Mtoto/Child Protection

UNHCR na washirika wake wa Kulinda Haki za Mtoto/Child Protection Danish Refugee Council (DRC) (Baraza la Wakimbizi la Denmark) wanatoa usimamizi wa kesi za Kulinda Haki za Mtoto/Child Protection huko Kakuma na Kalobeyei. Unaweza ripoti kesi za Kulinda Haki za Mtoto/Child Protection kwa DRC au unaweza kuwasiliana na UNHCR moja kwa moja.

Simu ya usaidizi wa shirika husika:

 • 0800720414 (DRC, bila malipo, ma saa 24)

Ofisi za Shirika la DRC kituo cha Kakuma

 • Kakuma 1, Z1 na 2 – Ofisi ya kulinda haki za mtoto, karibu na Kituo cha UNHCR cha Kakuma 1, kilichoko mkabala na ofisi ya NRC
 • Kakuma 1, Z3 na 4- Ofisi ya kulinda haki za mtoto, Social Service kilichoko mkabala na Don Bosco
 • Kakuma 2 na;3 – Kituo cha Furaha kilichoko karibu na shule ya upili ya Greenlight
 • Kakuma 3 – Kituo cha kulinda haki za mtoto eneo la kuwapokea wakimbizi wapya
 • Kakuma 4 – Ofisi ya DRC karibu na ofisi ya UNHCR kituo cha Kakuma 4 katika K4Z2B8
 • Kakuma 4 – Kituo cha Furaha 4, K4Z2B2

Ofisi za DRC kituo cha Kalobeyei:

 • Kijiji 1 – Kituo cha Furaha
 • Kijiji 1 – Ofisi ya kulinda haki za mtoto eneo la kuwapokea wakimbizi wapya
 • Kijiji 2 – Kituo cha Furaha 2
 • Kijiji 3 – CFS 3/DRC Kituo cha kuimarisha kina mama cha N17

Sehemu za kupendeza watoto (Vituo vya Furaha), zinazosimamiwa na DRC, hivi sasa zimefungwa kwa shughuli za kawaida za kucheza kwa sababu ya COVID-19; Walakini, shughuli zingine za usimamizi wa kesi bado zinaendelea. Watoto wamekuwa wakicheza nje ya vituo na wenzi wamekuwa wakishirikiana nao kwa kufuata miongozo ya kukaa kwa umbali sehemu ambapo wanacheza.

Kwa maelezo zaidi kuhusu ombi la vyeti vya kuzaliwa na usimamizi wa malezi, tafadhali tafuta ushauri wa kisheria na uandikishaji (documentation).


See also

<< Back to Kenya homepage >> Select another country on our Help page