UNHCR inafanya kazi na washirika wake Africa Inland Church Health Ministries (AICHM), International rescue Commitee(IRC) na Kenya Red Cross Society (KRCS) kutoa huduma za bure za afya kwa wakimbizi na wanao omba hifadhi na kwa wenyeji huko Kakuma na kalobeyei; wakiwa na vituo nane(8) vya afya katika kambi na makazi ya kalobeyei mukiwemo hospitali kuu moja ,vituo vikuu viwili na dispensari tano (ambazo zinajulikana kwa jina kliniki za afya).
Katika vituo vyote unaweza kupokea huduma zifwatazo:
- Utunzaji kamili wa msingi wa afya
- Huduma ya afya ya mama na motto mukiwemo;
- chanjo;
- matunzo ya mbele ya kuzaa;
- matunzo ya baada ya kuzaa
- mashauriano ya watoto
- Mashauriano ya watu wazima:
- Utambuzi na tiba ya magonjwa kama vile kuhara, homa ya mapafu, malaria, ugonjwa wa kisukari, shinikizo la dam una zinginezo
- Huduma za msingi za uuguzi
- Kuosha na kutunza vidonda
- Huduma msingi za maabara
- Vipimo vya haraka vya malaria, uchunguzi wa damu pamoja na viwango vya sukari ya damu na zinginezo
- Huduma za duka la dawa
- Utoaji wa dawa inayopatikana katika dawa muhimu za UNHCR na kwa orodha ya vifaa
- Huduma za kisakolojia kwa watu wenye shida ya afya ya kiakili
- Huduma kuhusu HIV/AIDs na kifua kikuu
- Vipimo, kutibu pia na mashauri
Zaidi ya hayo, hivo vituo viwili vikuu vina toa huduma za kuzalisha na zote mbili zina kata za uzazi/mataniti. Hospitali kuu ina toa huduma zote kwa wagonjwa pia wa kulazwa humo; kuna chumba cha upasuaji pia huduma za kuonesha picha(ultra sound na x-ray).
Jina | Linalojulikana pia kama | Aina | Shirika | Eneo | Saa za kufungua |
Hospitali Kuu ya Ammusait | Hospitali Kuu ya IRC | Hospitali | IRC | Kakuma 4 | Saa 24 |
Kituo cha Afya cha Kaapoka | Hospitali kuu ya Zamani | Kituo cha afya | IRC | Kakuma 1 | Saa 24 |
Kituo cha Afya cha Natukubenyo | Kituo cha Afya Kalobeyei | Kituo cha afya | KRCS | Kalobeyei v1 | Saa 24 |
kliniki ya Lochangamor | Kliniki ya Kliniki 4 | Zahanati/Kliniki | IRC | Kakuma 1 | 8 asubuhi – 3 jioni |
kliniki ya Hong Kong | Kliniki ya Kliniki 2 | Zahanati/Kliniki | IRC | Kakuma 1 | 8 asubuhi – 3 jioni |
Kliniki ya Nalemsokon | Kliniki ya Kliniki 5 | Zahanati/Kliniki | AIC | Kakuma 2 | 8 asubuhi – 3 jioni |
kliniki ya Nationokor | Kliniki ya Kliniki 6 | Zahanati/Kliniki | IRC | Kakuma 3 | 8 asubuhi – 3 jioni |
kliniki ya Naregae | Kliniki ya Kalobeyei Kijiji cha2 | Zahanati/Kliniki | AIC | Kalobeyei V2 | 8 asubuhi – 3 jioni |
Njia ya Rufaa
UNHCR na washirika wa afya wana njia zaidi ya rufaa na kupanga ziara za wajuzi wa wa matibabu kwa wagonjwa wanaohitaji utunzaji maalum. Wanaotafuta hifadhi na wakimbizi ambao wana hali ambayo inahitaji utunzaji maalum watarekodiwa katika msingi wa data ya rufaa na kusaidiwa wakati wataalam wanapofika kwenye misheni. Kesi nyingi zisizo za dharura huanguka katika kitengo hiki.
Kwa idadi ndogo ya kesi kulingana na hitaji la dharura la matibabu (kuokoa maisha au kuzuia ulemavu wa kudumu), UNHCR na washirika wa afya wanaweza kutuma watu kwa matibabu huko Lodwar au Nairobi.
Gari za wagonjwa
Gari mbili za wagonjwa zina hudumia Kakuma na gari moja ina hudumia Kalobeyei. Tafadhali pigia ambulensi kwa dharura za kuokoa maisha tu.
- Kakuma 1 – 0719105775 (IRC)
- Kakuma 2, 3, 4 – 0719105549 (IRC)
- Kalobeyei – 0707173515 (KRCS)